MISS TOURISM 2011-MARA ITAFANYIKA TAREHE 7 YA MWEZI UJAO

Hatimaye lile shindano la kumsaka mlimbwende wa mkoa wa Mara katika maswala ya utalii, litafanyika Ijumaa ya tarehe 07/10/2011, katika ukumbi wa Bwalo la Magereza mjini Musoma, ambapo takriban warembo 15 watapanda jukwaa moja kuchuana kumpata muakilishi wa mkoa katika mashindano ya Miss Tourism Lake Zone yatakayofanyika baadae mwezi december. 
 
Kampuni ya Stoppers Entertainment inayoandaa mashindano hayo, imejipanga kuyapa hadhi mashindano hayo ambapo warembo mbali na kupita jukwaani, watashiriki katika shughuli za kijamii, kuimba na kucheza ngoma za makabila ya mkoa wa Mara. Hata hivyo waandaji wamewaomba wadhamini kuendelea kujitokeza kudhamini shindano hilo, kutokana na kugusa utalii, utamaduni na uchumi wa nchi yetu, yote kwa minaajili ya kuitangaza Tanzania. 
 
Shindano la Miss Tourism Mara 2011, litasindikizwa na burudani kutoka kwa Ditto na Linah wote kutoka jumba la vipaji THT. Pia burudani za ngoma za asili zitakuwepo.

Posted by Bigie on 11:23 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.