HAYA NDO MAKAMUZI YA AKUDO USIKU WA KUAMKIA LEO

Prezdaa Msaidizi wa Akudo, Tarcis Masela (katikati) akiserebuka pamoja wanenguaji wa bendi hiyo.
Mfanyabiashara  wa Mitumba katika Soko la Makumbusho, Pius Ruta ‘Mzee wa Pamba’ (kulia) akimwagia wekundu wa msimbazi Prezdaa wa bendi hiyo, Christian Bella.
 
Kinadada wakienda kumtunza, Tarcis Masela.
 
Mkurugenzi Mkuu na mwanamuziki wa Kundi la East African Melody Modern Taarab, Haji Mohammed akiwapagawisha mashabiki leo alfajili.
 
Muimbaji mkongwe wa taarab, Afua Suleiman akifanya makamuzi kwenye onesho hilo.
 
Haji Mohammed akiimba kwa hisia kali.
 Bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’ usiku wa kuamkia leo ilinaswa na kamera yetu ikifanya makamuzi kwenye Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es Salaam ambapo kundi la Taarabu la East Africa Melody lilinaswa likikamua kwenye Hoteli ya Travertine jijini Dar.

Posted by Bigie on 5:42 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.