HIVI NDIVYO CCM INAVYOTAMBA HUKO IGUNGA

Vijana wa Ipumbulya kata ya Bukoko wakiomba kwa hamu kushika mkono wa mgombea ubunge jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM, Dk. Dalaly Kafumu, katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika kijiji hicho, jana.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Asha Abdallah Juma akimwombea kura mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Dk. Dalaly Kafumu katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika jana katika kijiji cha Ipumbulya Kata ya Bukoko ,jimbo la Igunga mkoani Tabora.
Msanii wa kundi la Tanzania One Theatre (TOT) Khadija Kopa (ushoto) akifanya mamnjonjo yake, kundi hilo lilipotumbuiza jana katika mkutano wa kampeni za CCM jimbo la Igunga, kwenye Kijiji cha Ipumbulya kata ya Bukoko mkoani Tabora.
. Mkazi wa Ipumbulya akiwa amembeba mtoto wake begani apate kumuona mgombea ubunge jimbo la Igunga, Dk. Dalaly Kafumu katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji Kata ya Bukoko jana.
Wananchi wakishangilia wakati Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Steven Wasira alipokuwa akimtambulisha mgombea wa Ubunge jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM, Dk. Dalaly Kafumu katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kijiji cha Ipumbulya Kata ya Bukoko, Igunga mkoani Tabora, jana.

Posted by Bigie on 2:00 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.