JUMA NATURE AAMUA KURUDIANA NA SINTAH. VIPI JUU YA FAMILIA NA MKE WAKE?
JAMII 6:08 AM
Kweli adui mpenzi ni laini kwa nyama ya ulimi, wawili wanaopendana kwa dhati hawaachani ila hupumzishana kupisha hasira ziishe, kuhusu mastaa Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’ na Christine John Manongi ‘Sintah’ ni stori ya MV Mapenzi.
Habari zinasema kuwa Nature na Sintah hivi sasa hawana bifu, wamesahau tofauti zao, wapo pamoja hivyo kuibua ‘ndogo ndogo’ kwamba wamerudiana tena baada ya bifu la miaka tisa.
WAPEKUZI tunajua kuwa Nature ni mume wa mtu lakini tumenasa mazungumzo yake na Sintah ambayo yanatengeneza picha kuwa ama wamerudiana kweli au kuna kitu kinaendelea kati yao.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa Nature na Sintah hivi sasa wanawasiliana kwa kiwango ambacho kinadhihirisha jinsi wanavyoelewana.
wapekuzi , walifanya kazi yao kikamilifu na kunasa mazungumzo ya hapa na pale kati ya mastaa hao .
Sintah alisema: “Sijawahi kuwa na uadui na Nature, sihitaji kuzungumza yaliyopita lakini kwa sasa ni kweli tunawasiliana vizuri kwa sababu tunataka kufanya kazi pamoja.
“Kuna filamu tunacheza pamoja, inaitwa Sitaki Demu. Kwa hiyo mimi na Nature ni marafiki kikazi. Kuhusu mapenzi hapana, namheshimu sana Nature, yule ni mume wa mtu, namheshimu sana mke wake. Nami nina mtu wangu, nampenda na kumheshimu sana.”
Nature alisema: “Tunatengeneza filamu, kwa sasa tumesimama, Sintah yupo busy na kazi zake, akishakaa sawa tutakamilisha filamu. Ni kazi tu, hakuna kingine.”

HISTORIA YAO YA NYUMA
Nature na Sintah walizama kwenye penzi zito mpaka kutangaza kufunga ndoa lakini mwaka 2002 waliachana, huku mwanamuziki huyo akimtuhumu mwenzake kwa kutokuwa mwaminifu.
Baada ya kuachana, kikapita kipindi cha bifu ambapo Nature alidaiwa kurekodi nyimbo mfululizo akieleza madudu ya Sintah. Ngoma hizo ni Sitaki Demu (Original na Remix) pamoja na Inaniuma Sana.
Mwaka 2003, wakati Nature akiwa kwenye ziara ya muziki Mwanza, Sintah alipanda jukwaani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na kucheza wimbo Sitaki Demu.
Nature ambaye alikuwa anaimba, baada ya kumuona Sintah akicheza jukwaani alisusa kuimba, hivyo kutibua shoo hiyo ambayo ilikuwa imeandaliwa na Prime Time Promotion ambayo ni kampuni tanzu ya Clouds Media Group.
Wakati huo, Sintah alikuwa mtangazaji wa Redio ya Watu, Clouds FM, Mwanza na kutokana na tukio hilo la kuhusika kuharibu shoo ya Nature, menejimenti ya redio hiyo, chini ya Mkurugenzi Mtendaji, Joseph Kusaga, iliamua kumfukuza kazi.