JINI KABULA AMKIMBIA " MR.NICE " NA KUOLEWA NA MWANAMKE MWENZIE. ADAI WANAUME HAWAMRIDHISHI

Hakika ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni, msanii wa  filamu za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’  (pichani) ametoa kali ya mwaka baada ya kutimka kwa mpenzi wake mwanamuziki, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ na kwenda kuwekwa kinyumba na mwanamke mwenzake Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam

Habari zilizonaswa na chanzo chetu zinasema kwamba, Jini Kabula alihama kwa mpenzi wake huyo maeneo ya Kawe jijini Dar na  kwenda kwa mwanamke mwenzake kwa sababu ya kuridhishwa  kimapenzi.
Mara baada ya kuzipata taarifa hizo, mpekuzi wetu alipiga hatua hadi Tabata kuthibitisha juu ya habari hizo lakini alipofika  sehemu aliyoelekezwa, hakumkuta na kuambiwa kuwa amekwenda kazini.

“Ni kweli Jini Kabula anaishi hapa lakini ukitaka kumpata nenda saluni ya Mercy Hygienic Classic Barber pale Mawenzi Savana, utamkuta amepata ajira pale,” alisema jirani huyo.
mpekuzi  wetu alifika hadi Mercy saluni na  kumkuta  Jini Kabula akiwa ‘bize’ akimsafisha uso ‘scrub’  mteja , mara alipomaliza kazi hiyo mwandishi wetu alimtupia tuhuma za kuhamia kwa mwanamke, ndipo msanii huyo alipofunguka na kulimwagia sifa penzi hilo analolipata kutoka kwa mwanamke mwenzake.

“Kwani kuna matatizo gani mimi kuhamia kwa mwanamke mwenzangu, kama ni mapenzi basi mjue kuwa nyie wanaume mmeshindwa kuniridhisha ndiyo maana nimehamia huku,” alisema  Jini Kabula.
Msanii huyo alimshukuru Mungu kwa kuwa mwanamke mwenzake ameweza kumtuliza na kumtafutia kazi, hivyo hana haja ya kuhangaika na wanaume kwa sasa. 

Posted by Bigie on 5:38 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.