PNC F/ PROF.JAY AND CHID BENZ- YOU ARE THE ONLY ONE


Kimsingi wimbo huu nilitakiwa niuweke hapa takribani wiki nne zilizopita kwani ndio uliingia rasmi mitaani yaani katika radio stations mbalimbali hapa Afrika Mashariki na Kati.Then maisha,ups and downs,nikachelewa kidogo.Lakini kama wenzetu walami wanavyosema, better late than never.
Ni wimbo mpya kutoka kwa msanii PNC ambaye kwa kumsikiliza tu utagundua kwamba ni msanii mwenye uwezo wa hali ya juu katika kuimba.Katika wimbo huu,PNC amewashirikisha Professor Jay na Chidi Benz ambao sote tunajua uwezo wao katika kuzitendea haki beats na mirindimo hususani kwenye mahadhi ya hip-hop.
Wimbo umefanyiwa pale Burn Records mitaa ya Tabata chini ya Producer Sheddy Clever ambaye ni kijana anayekuja juu kwa kasi ya ajabu katika masuala mazima ya production.Usikilize You Are The Only One hapo chini


Pichani juu ni PNC(kulia) akiwa na Professor Jay ndani ya Burn Records mara tu baada ya kukamilisha You Are The Only One.

Posted by Bigie on 3:28 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.