UJIO WA FILAM YA DR.THOMAS....KAA MKAO WA KULA
JAMII 3:01 AM
Loveness Watson
Mrembo anayekuja juu katika tasnia ya filamu Tanzania Loveness Watson anatarajia kuachia filamu mpya inayokwenda kwa jina la Dr. Thomas, filamu hiyo ipo tayari kwa ajili ya kusambazwa na itasambazwa nchi nzima ili kila mpenda filamu waione.
“Katika filamu zangu hii ni nzuri kupita maelezo, na nimetayarisha mwenyewe kwa kushirikiana na ndugu yangu katika kutengeneza, kwa sasa nimejitoa kufanya kazi kwa nguvu zaidi na kwenda mbele katika tasnia ya filamu nyumbani, Dr. Thomas ni filamu ya aina yake,” alisema Loveness.
Msanii huyu hadi sasa ameshiriki filamu nyingi kama vile Blood in the City, Sheria mkononi, Penzi la utata, The Game, Uzio wa kuzimu, Kafala ya Damu, Fake Love, Impossible Promise na Dr. Thomas, pia Loveness ni mtayarishaji wa filamu akishirikiana na King Rich Production.






