WABUNGE NA WAANDAMANAJI WAMPINGA POPE BENEDICT XVI HUKO UJERUMANI

Mtakatifu Pope Benedict xvi akihutubia Bunge.

Kiongozi wa kidini wa kanisa la Kikatoliki duniani Mtakatifu Pope Benedict xvi (Joseph Ratzinger),amejikuta yupo katika mvutano mkubwa na wanasiasa nchini ujerumani,baada ya wabunge wapatao 100 kutoka nje ya bunge la ujerumani wakati Pope Benedict akiwa analihutubia bunge la nchi hiyo (Bundestage) majira ya alasiri ya alhamisi (22-09-2011) mjini Berlin,ambako Baba mtakatifu yupo akiendelea na ziarani nchini hiyo ya Ujerumani.

Wabunge hao walimsusia Pope na kutoka nje ya bunge ambako walijumuhika na waandamaji wa wengine waliokuwa wanampinga Pope kuwepo katika ukumbi huo wa bunge hilo.

Habari za kuaminika na za uhakika zinaeleza kuwa baadhi ya wanasiasa na wabunge nchini ujerumani hawakubaliani na taratibu za uongozi wa Pope ,haswa linapokuja swala la matumizi ya KONDOMU,kwani kanisa la kikatoliki halikubaliani na matumizi ya kondomu,pia sababu zingine za kupingwa kwa Pope nchini ujerumani ni pamoja kashfa zinazowagusa baadhi ya watumishi wa kanisa la kikatoliki duniani kwa kuhusika na kuwafanyia vitendo vichafu watoto au vijana katika miaka ya nyuma.

Pope Benedict amekuwa muwazi na kuwahi mara nyingi kuomba radhi hadharani kwa niaba ya kanisa lake,lakini wakosoaji bado wanaendeleza nongwa ! sababu nyingine ya wanaopinga kulihutubia bunge la Ujerumani ni kuwa DINI NA SIASA ni vitu viwili tofouti kwa maana hii Pope Benedict xvi (Joseph Ratzinger) hapaswi kuwepo ndani ya jumba la bunge au kulihutubia bunge ambalo ndilo baraza la kutunga sheria.

Pope Benedict xvi ni mzaliwa wa Ujerumani,ambapo alizaliwa kwa jina la Joseph Ratzinger ,huko Bayern,Ujerumani ya kusini.

Vyombo vya habari nchini ujerumani vimetonya kuwa kuanzia mwaka 2010 wafuasi wapatao 160,000 wa kanisa la kikatoliki nchini Ujerumani wamelihama kanisa hilo na kujiunga na madhehebu mengine.

Posted by Bigie on 8:51 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.