CHRISTINA SHUSHO ATEULIWA KUWA MHUDUM WA SEMINA KATIKA CONFERENCE ITAKAYOFANYIKA COLLAGE PARK-MAREKANI


Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili hapa Tanzania na sasa Afrika Mashariki na penginepo duniani atakuwa mmojawapo wa wahudumu wa semina na ‘conference’ itakayofanyika College Park, Maryland Marekani kati ya tarehe 3 - 9 Oktoba 2011. Kwa habari zaidi kuhusu huduma hiyo tafadhali tembelea hapa: http://thewayofthecrossgospelministries.org/upcoming-events-page
Christina Shusho ametoa albam mbili mwaka huu 2011 zijulikanazo kama ‘Nipe Macho’ na ‘Kwa la Kanisa Kristo’ na zinapatikana kwa viwango vya audio (CD). Kwa wale walioko Marekani na Canada inawezekana wakapata Video za mojawapo ya albamu hizo wakati wa ziara hii kama zitakuwa zimekamilika.

Christina Shusho ni mtumishi wa Mungu na amekuwa baraka sana popote alipohudumia. Kwa hiyo Marekani na Canada kaeni tayari kupokea baraka zake wakati wa conference hii. Inawezekana kabisa akatembelea pia state nyingine kama Texas (Houston na Dallas). Hii haijahakikishwa, mtafahamishwa habari zaidi zikipatikana.

Posted by Bigie on 9:14 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.