WASANII WA KUNDI LA MUTATI TOKA KENYA WATUA DAR ES SALAAM LEO


Wasanii wa miondoko ya Salsa wa kundi la Mutati la nchini Kenya wakiwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, wasanii hao wataburudisha katika hafla ya Shear Ball itakayofanyika Jumamosi katika Hoteli ya Movenpick.Hafla hiyo inalenga kuchangisha milioni 50 za kusaidia ukarabati wa mfumo wa maji taka katika hospitali ya Mwananyamala pamoja na kusaidia fedha za matibabu kwa wanawake wenye kuugua ugonjwa wa fistula.
Mkuu wa Masoko na Kitengo cha Uhusiano wa Kampuni ya Shear Illusion,Dorah Raymond akimkabidhi maua mmoja kati ya wanamuziki wa kundi la Mutati mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Mwalimu Nyerere.
Wasanii wa kundi la Mutati wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Masoko na Kitengo cha Uhusiano wa Kampuni ya Shear Illusion,Dorah Raymond (wa pili kushoto).

Posted by Bigie on 7:46 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.