ASIA NA AFRIKA ZAUNGANA KUANZISHA MPANGO WA PAMOJA WA KUMSOMESHA MWANAMKE
Posted by Bigie
JAMII
6:12 PM
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akihutubia Mkutano wa Afrika-Asia 2011 jana ambapo amesisitiza elimu yenye maadili ndiyo njia pekee ya kumkomboa mwanamke pamoja na jamii kwa ujumla. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Wanawake cha Sookmyung nchini Korea Kusini ambacho kimetiza miaka mia moja na tano tangu kianzishwe 1906.
Picha ya pamoja ya Viongozi wa ngazi ya juu kutoka Afrika na Asia waliohudhuria mkutano huo
Baadaye Spika Makinda alipata wasaa wa kukutana na vyombo vya habari na kufafanua umuhimu wa kuwa na vyuo vikuu vya wanawake. Hapa anaongena Avivang Tv ya Korea
Salma Dinya ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John Dodoma ambaye alialikwa kwenye mkutano huo kuiwakilisha Tanzania kama kiongozi kijana. Hapa anatoa mada kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Asia na Afrika kuhusu Tanzania.
Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Korea katika Vyuo Vikuu mbalimbali walifika kumsiliza spika wao
Spika wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwa na mwenyeji wake Dkt Han, Rais wa Chuo Kikuu cha wanawake cha Sookmyung, Korea
Wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali Asia na Afrika wakimsikiliza Bi. Salma DinyaKwa picha na matukio zaidi tembelea

Posted by Bigie
on 6:12 PM.
Filed under
JAMII
.
You can follow any responses to this entry through the
RSS 2.0