BABA MWENYE NYUMBA AAMUA KUWATIMUA WAPANGAJI KWA KUTOA VITU VYAO NJE BAADA YA KUTOLIPWA KODI YA NYMBA KWA MIAKA MITATU
JAMII 2:17 PM
Haya ndio Maandishi yaonekanayo kwenye kuta ya nyumba hiyo iliopo katika makutanao ya Mtaa wa Kariakoo na Jangwani,jijini Dar es Salaam.
Mzee mwenye nyumba hiyo afahamikae kwa jina la Mzee NYUMBA (kushoto) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo la tukio jioni ya leo,juu ya nia yake ya kuwatoa wapangaji wake wote waliokuwepo kwenye nyumba yake hiyo kwa madai ya kutolipia kodi ya pango kwa kipindi cha miaka mitatu.
Hali hiyo imekuja kutokana na Mzee huyo kupewa kibali maalum na Mahakama baada ya kushinda kesi dhidi ya mtu aliekuwa akisema ndie mwenye nyumba na kuamua kuwaondoa wapangaji wake wote katika nyumba hiyo.Kwa Upande wa Wapangaji wa Nyumba hiyo walieleza kwamba wao hawakukaa katika nyumba hiyo bila ya kulipa kodi,kwani kuna Mtu ambaye aliwapangisha (hawakumtaja jina) kuwa ndie aliekuwa akichukua Kodi zao kwa kipindi chote hicho.Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Mtaa Huo,Mzee Kasim (katikati) pamoja na majirani waliokuwepo eneo hilo.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Mbinga Auction Mart wakiendelea na jukumu walilopewa la kutoa vyombo vya wapangaji wote waliokuwepo katika nyumba hiyo.
Vyombo vikiwa vimetolewa nje ya nyumba hiyo.
Jamaa Mbinga Auction Mart hanawa Masihara hata kidogo katika katika jukumu hili.
Vyombo vikiwa nje.