TAIFA STARS IMEONDOKA KUELEKEA MOROCCO KWA AJILI YA MCHEZO WAO WA JUMAPILI
JAMII 2:28 PM
Kocha wa Taifa Stars Jan Poulsen akielekea kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere jioni ya leo wakati timu hiyo ikiondoka kuelekea Morocco
![]() | |
| Baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars wakijiandaa jioni ya alhamisi kwenye uwanja wa Kimataifa wa JK Nyerere kuelekea nchini Morocco. |
Timu ya taifa 'Taifa Stars', Alhamisi jioni imeondoka nchini kuelekea nchini Morocco ,kwa ajili ya mchezo wao utakaofanyika jumapili kukamilisha mchezo wa mwisho wa kundi D kwa kunyukana na timu ya Morocco,katika mji wa Marrakech nchini humo,katika kuhakikisha timu hiyo inafuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika, mwakani (CAN 2012).
Aidha katika kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa kwa Taifa Stars,Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), imetoa sh. milioni 165 kwa ajili ya safari ya timu hiyo,ambapo fedha hizo zimetokana na vifaa, nauli ya kwenda na kurudi na gharama zingine za timu hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Emphraim Mafuru alisema kampuni yake kwa miaka mitano mfululizo imedhamini timu za taifa zikiwemo za vijana na wanawake, hivyo wataendelea kufanya hivyo.Alisema katika kuhakikisha Stars inafanya vizuri wametoa sh. milioni 165 kwa ajili ya vifaa vya mazoezi, zikiwemo jezi na viatu, nauli ya kwenda na kurudi Morocco pamoja na gharama zingine za safari hiyo na kwamba anawaomba Watanzania, waiombee timu hiyo ili itoke na ushindi.








