BARAZA LA VIONGOZI WA DINI LA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA LITAZINDULIWA TAREHE 11 YA MWEI HUU


Viongozi wa Dini Mbalimbali wakiwa katika picha  ya pamoja na Waratibu kutoka TUME,Wizara ya Afya,Taasisi ya AIHA pamoja na Taasisi CDC.

Ili kukabiliana na matumizi haramu ya dawa za kulevya, Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeratibu uanzishwaji wa Baraza la Viongozi wa Dini la Kupambana na Dawa za Kulevya.

Baraza hili linaundwa na wajumbe Kumi na nne,wajumbe saba kutoka katika taasisi za Kikiristo na wajumbe saba kutoka katika taasisi za Kiislamu.

Jukumu la Baraza hili litakuwa ni kusimamia utoaji wa huduma za kiroho kwa watumiaji wa dawa za kulevya wanaopata nafuu na kutoa elimu kwa vijana kuhusiana na kujikinga na matumizi haramu ya dawa za kulevya katika taasisi zao na jamii yote kwa ujumla.

 Uanzishwaji wa Baraza hili umefadhiliwa na Serikali ya watu wa Marekani Kupitia Centers for Disease Control and Prevention (CDC) pamoja na taasisi ya American International Health Alliance (AIHA).

Baraza hilo litazinduliwa Rasmi tarehe 11 Oktoba mwaka 2011, katika hoteli ya Hilton Double Tree, Masaki, Dar es Salaam kuanzia saa tatu na nusu asubuhi.Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi.

Posted by Bigie on 4:29 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.