BINTI MLEMAVU ASAIDIWA KIASI CHA Th. 800,000 LEO NA MSAMARIA MWEMA
JAMII 6:28 AM
Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds Media Group Ltd BI JOYCE SHEBE akimkabidhi kiasi cha fedha taslimu shilingi 800,000/- zilizotolewa na msamalia mwema kwa Mlemavu Frida Kavishe alizoomba kwa ajili ya kulipia ada ya masomo ya Shahada ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Anayeshuhudia ni kaka wa Frida, Omari Mkete.
Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds Media Group Ltd BI JOYCE SHEBE akizungumza baada ya kukabidhi kiasi cha fedha taslimu shilingi 800,000/ zilizotolewa na msamalia mwema kwa Mlemavu Frida Kavishe (Kushoto) kwa ajili ya kulipia ada ya masomo ya Shahada ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Katikati ni kaka wa Frida, Omari Mkete.
Baadhi ya watendaji wa chumba cha habari Clouds FM/TV kutoka kushoto Shaffih Dauda, Sophia Kessy, Jackie Kombe, Joyce Shebe, Jerome Risasi na Juma Katunda wakiwa kwenye picha ya pamoja na Frida Kavishe na Omari Mkete mara baada ya makabidhiano ya fedha hizo.








