TRANSFORMER YA TBC YALIPUKA TENA KWA MARA NYINGINE
JAMII 6:21 AM
TRANSFOMA iliyoripuka juzi Jumanne na kuwahiwa kuzimwa, imeripuka tena muda uliopita na kuhatarisha kuungua kwa ofisi za TBC na Star Times! Taransfoma hiyo mali ya Tanesco, iko usoni kabisa mwa ofisi za Star Times zilizopo jirani na studio za TBC barabara ya Bagamoyo, eneo la Bamaga. Juzi walikuwepo mafundi wa Tanesco wakitengeneza transfoma hiyo ndipo moto ulipomripukia fundi aliyekuwa akitengeneza ambaye alikimbizwa hospitali na kisha moto kuwahiwa kuzimwa na wafanyakazi wa Star Times wenye asili ya China kwa kutumia Fire Extinguishers. Leo moto huo ulizuka wakati wa jaribio la kuliwasha transfoma jipya lililofungwa baada ya lile la mwanzo kuungua.








