CHADEMA WAJIANDAA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI WA IGUNGA


   Chama chadema kimegomea matokeo ya ubunge jimbo la Igunga ambapo wanadai kuna vitu ambavyo havijaenda sawa,hivyo kimekimejipanga kufanya mapinduzi ya kidemokrasia na muda si mrefu wataongea na vyombo vya habari.
   Kongozi wa  chama hiko amesema CHADEMA hakijasaini kukubali matokeo siku ya leo,hata hivyo mgombe wa CUFamejikuta anaangukia pua mbali ya kuwa mgombea bora kwa sera za kueleweka vituo kibao amepata maziro yakumwaga.
     Mgombea kupitia  Chama cha Mapinduzi   CCM Dokta Dalaly Kafumu  ameshinda uchaguzi wa  ubunge  katika jimbo la Igunga mkoani Tabora.
     Msimamizi wa uchaguzi   Protase Magayane     akitangaza  matokeo hayo amesema.
Kuwa  Dokta Kafumu amepata kura elfu 26434 dhidi ya mpinzani  wake  Joseph Kashindye wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema  aliyepata kura elfu 23 260.
     Amesema  kura zilizopigwa zilikuwa ni elf 53 672  ambapo kura halali ni  elfu 52 487  na zilizoharibika ni  kura elfu 1185.

     Aidha  msimamizi huyo amesema kuwa  jumla ya wapiga kura waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ni laki   17077.

Posted by Bigie on 8:45 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.