JUMLYA YA KAYA 80 JIJINI MWANZA HAZINA MAKAZI BAADA YA " MKUMBO WA BOMOA BOMOA "
JAMII 7:19 AM
Zaidi ya kaya 80 katika Mtaa wa Ghana jijini Mwanza hazina mahali pa kuishi kutokana na Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza jana majira ya saa 3 asubuhi kubomoa nyumba walizokuwa wanaishi ili kupisha ujenzi wa mradi wa Jengo la Machinga Complex.
Kwa siku ya leo imekuwa ni kama mwendelezo watu waliokuwa wakiishi katika nyumba hizo wameonekana wakihangaika huku na kule kuhamisha vifaa vyao kutoka katika nyumba hizo.
Wengine wakifanya mikakati ya kuhamahama kabla ghalika hajafika.
Kutokana na bomoa bomoa inayoendelea Eneo la Ghana kwa sasa limekatiwa umeme hali inayosababisha ulinzi wa mali kuwa mgumu, usiku mzima wananchi hao wamekesha kulinda mali zao kwani vibaka walikuwa wakilandalanda kuiba mali zilizonje ya magofu ya nyumba zilizobomolewa sambamba na kung’oa flemu za milango na madirisha.
Wananchi hao wameiomba serikali kuwapatia maturubai kwa ajili ya kujisitiri wakati wakiwa katika harakati ya kutafuta sehemu nyingine ya kupanga






