MBUNGE WA MBARALI MKOANI MBEYA (CCM) AFIKISHWA MAHAKAMANI



Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Mbarali Modestus Kilufi siku alipokuwa akikamatwa na polisi mwishoni mwa wiki.
Mbunge Kilufi(kushoto) akifikishwa mahakama ya mkoa jijini Mbeya

Mbunge wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya Modestus Kilufi (51) (CCM) aliyekamatwa mwishoni mwa wiki kwa kosa la kutishia kuzuru kwa kutumia silaha amepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Hakimu mfawidhi wa wilaya ya Mbeya na kunyimwa dhamana.

Wakisoma mashitaka mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Michael Mteite, Mawakili watatu wa Serikali Griffini Mwakapeje, Basilius Namkambe na Emma Msofe, wamesema kuwa Mbunge huyo alimtishia kumzuru Jordan Masweve March 16 mwaka huu wilayani Mbarali.

Wamesema kuwa kosa hilo ni kinyume na kifungu cha sheria 89 cha mabadiliko ya sheria ya mwaka 2002 kifungu kidogo cha 2(a) sura ya 16 ambapo mshitakiwa alikana shitaka.

Kesi hiyo yenye namba CC/158/2011 baada ya mshitakiwa kukana shitaka linalomkabili, ndipo wakili wa Mbunge huyo Simon Mwakolo aliiomba mahakama hiyo dhamana kwa mteja wake.

Baada ya ombi hilo kusikilizwa na mahakama, Hakimu Mteite alikataa ombi hilo na kwamba mtuhumiwa atatakiwa kepelekwa mahabusu hadi Octoba 24 mwaka huu wakati Mahakama ikiendelea kufikiria masharti ya dhamana.

Baada ya hapo kesi ikaahirishwa na Mbunge huyo kupelekwa mahabusu katika gereza la Ruanda lililopo mkoani Mbeya.

Posted by Bigie on 11:41 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.