MISS KINONDONI AKIRI KUWA ANA UHUSIANO NA STAA WA ORIGINAL COMMEDY- "VENGU"


Miss Kinondoni 2011 ambaye  pia aliingia Top 15 ya Miss Tanzania, Stella Mbunge amekiri kutoka na mchekeshaji wa Kundi la Orijino Komedi, Joseph Shamba ‘Vengu’
Akijibu swali la MPEKUZI wetu juzikati baada ya kumuuliza kuhusu tetesi zilizozagaa kuwa yeye na Vengu ni wapenzi na kwamba hivi karibuni msanii huyo alipoanza kuumwa alikwenda mara moja tu hospitalini kumpa ‘hi’, akijitetea yupo bize, Stella alifunguka:

Ni kweli mimi na Vengu ni wapenzi tena kwa muda mrefu, nadhani miaka mitano sasa. Kutokwenda hospitali mara kwa mara ni kwa sababu nilikuwa bize sana na kambi ya Miss Tanzania, hivyo nilikuwa napata muda mchache wa kutoka, lakini si kwamba nimemtenga,” alisema mlimwende huyo.

Hata hivyo, MPEKUZI wetu alipomuuliza wana malengo gani hapo baadaye kufuatia uhusiano wao wa kimapenzi, mnyange huyo alisema:

“Unajua uhusiano wetu pande zote mbili wanajua, hivyo tuombe Mungu atuepushe na ibilisi asijitokeze kuuharibu kwani malengo yetu ni kuoana na si kuchezeana.”

Aidha, Stella alisema tangu amalize kambi ya Miss Tanzania, yupo nyumbani kwa wazazi wake, Mikumi Morogoro kwa ajili ya mapumziko na pia alithibitisha kwamba hali ya Vengu imeanza kuimarika tofauti na ilivyokuwa awali.

Posted by Bigie on 5:47 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.