NINI HATIMA YA WEMA SEPETU MASAA MACHACHE YAJAYO? JE ATAACHIKA "LEO" AU ATAVISHWA PETE?


Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’ amesababisha viulizo vingi kwa tangazo lake la ‘sapraizi’ aliyoahidi kumfanyia mpenzi wake, Wema Isaac Sepetu.

Kwa tangazo hilo, kuna watu wanadai kuwa Diamond anataka kumpiga chini Wema, wengine wanasema atamvalisha pete ya uchumba, huku kundi la tatu likiamini ni sapraizi ya kumlipia mahari.

Diamond, amemsisitizia MPEKUZI wetu  kuwa Oktoba Pili, 2011 (LEO) atamfanyia bonge la sapraizi Wema lakini amekataa kuitaja kama ni kumuacha, kumvalisha pete au mahari.

Badala yake, Diamond amesema kuwa siku ya leo , atakuwa mwenye furaha ya hali ya juu na atatoa shoo ya kiwango cha juu kusindikiza sapraizi yake kwa Wema huku akiwaalika waandishi wa habari na watu maarufu kwa lengo la kuwaambia uamuzi wake.

Tunazo  data kuwa Diamond atakuwa anasherehekea kutimiza miaka 22  leo , hivyo amesema kuwa atasindikiza furaha yake kwa kumfanyia Wema kisichotarajiwa na wengi.

Diamond ‘Rais wa Wasafi’, alisema kuwa atafanya tukio ‘bab’kubwa’ kwenye Klabu ya New Maisha, Masaki, Dar es Salaam na amealika mastaa kibao.

Alifunguka: “Itakuwa ni pati ya kihistoria, mbali na kukata keki kubwa, mashabiki wangu wata-enjoy kwani kutakuwa na bata za kila aina.”

Alisema, wanamuziki Rashid Makwilo ‘Chid Benz’, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’, Hemed Suleiman na Shetta, watakuwepo pamoja na warembo kibao wa Bongo Movies. 

Hata hivyo, alipoulizwa anataka kumfanyia nini Wema kwenye ‘pati’ hiyo, Diamond alijibu: “Ni ‘sapraizi’, itakuwa wazi kwa kila mtu lakini sisemi nitamfanyia nini.”

Posted by Bigie on 6:04 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.