MWANAMKE AFARIKI BAADA YA KULAZIMISHWA KUNYWA SUMU NA MUMEWE KISA KIKIWA NI UPOTEVU WA SH. 450,000
JAMII 5:35 PM
Mtuhumiwa Bwana Mohamed Mwawipa (kushoto) ambaye anatuhumiwa kumshinikiza mkewe Nuru Masuba kunywa sumu baada ya kumtuhumu kuwa amemwibia fedha taslimu shilingi laki nne na elfu hamsini akionesha askari wa upelelezi eneo alilonywea sumu mkewe
Mwenyekiti wa kijiji cha Ijumbi kata ya Ruiwa wilaya ya Mbrali Bwana John Mkalimoyo akimfariji dada wa marehemu Nuru Masuba aitwaye Stumai Wilson ambapo marehemu alikuwa akiishi naye Kijiji cha Mapogolo kapunga.
HABARI KAMILI
Mohamed Mwawipa mwenye Umri wa miaka 50 mkazi wa kijiji cha Ijumbi kata ya Luwiwa wilayani Mbarali mkoani Mbeya anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa tuhuma za kumshinikiza mkewe kunywa sumu baada ya kumtuhumu kumwibia shilingi laki nne na elfu hamsini.
Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa marehemu Nuru Mwasuba alikuwa na ugomvi kwa kipindi kirefu na mumewe hali iliyopelekea wakatengana lakini October 4 walirejeana upya mahusiano yao hadi kifo kilipomfika.
Akiongelea tukio hilo mwenyekiti wa kijiji cha Ijumbi John Kalikumoyo amesema mtuhumiwa alikiri kutenda tukio baada ya kuhojiwa na uongozi wa kijiji na kwamba endapo mwanamke huyo asigekubali kunywa sumu angetumia silaha ya jadi aina ya kisu kumuangamiza kama fedha hizo hazitoonekana.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alipoulizwa juu ya kukamatwa kwa Mohamedi Mwawipa alisema kuwa taarifa hizo bado hazijamfikia na kwamba atazitolea ufafanuzi pindi atakapo pata taarifa kamili kutoka kwa mkuu wa polisi wilaya ya Mbarali.
SOURCE: MBEYA YETU






