NAIBU WAZIRI WA ELIMU AWAASA WANANCHI WA JIMBO LAKE LA SONGWE WILAYANI CHUNYA KUTOTEGEMEA KILIMO CHA TUMBAKU PEKEE
JAMII 5:48 PM
WAKULIMA na wananchi wa bonde la Songwe Wilayani Chunya Mkoani Mbeya wametakiwa kuacha kutegemea kilimo cha zao la Tumbaku pekee na badala yake kubadilika na kuanza kulima mazao mchanganyiko ya biashara na kilimo.
MPEKUZI wetu anaripoti kuwa ,Imeelezwa kuwa wakulima wa bonde hilo bado wana dhana ya kutegemea kilimo cha tumbaku pekee wakati kuna mazao mengine wanaweza kulima na kufanya biashara zao kwa uhakika zaidi Chakula ili kuepukana na aathari wanayoipata kwa hivi sasa kutokana na tatizo la soko la zao la Tumbaku.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mbunge wa jimbo la Songwe na Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi Bw.Philipo Mulugo wakati alipokuwa akizungumza na Wananchi maeneo mbali mbali katika mikutano ya hadhara.
Hatua ya Mbunge huyo kutoa wito huo imekuja baada ya wananachi na Wakulima wa zao la tumbaku kutoa malalamiko yao kuwa hadi sasa bado hawajalipwa fedha zao za tumbaku huku wengine wakidai kuwa tumbaku hiyo imejaa kwenye maghala kutokana na kukosa mnunuzi.
Bw.Mulugo alisema kuwa tatizo la soko la tumbaku ni la nchi nzima na kwamba serikali inaendelea kulishughulikia na kusimamia wanunuzi waliochukua tumbaku ya wakulima kuwalipa fedha zao mapema ili kuwasaidia wakulima kuweze kuendesha maisha yao.
“Huku kwetu kuna mazao mengi ya biashara mbayo yanakubali kustawi na mazao hayo ni kama,ufuta ulezi,maharagwe,Mahindi,na matunda aina ya maembe ambayo nina uhakika wa kupata soko lake kwani tayari kuna mnunuzi wa matunda hayo na anayahitaji kwa wingi alisema”alisema
Hata hivyo katika taarifa za vijiji katika jimbo hilo wakulima hao walimuomba mbunge huyo kuwasaidia kupata fedha zao za tumbaku kwa kuwashinikiza wanunuzi kuwalipa fedha hizo na kuwatafutia masoko ya uhakika kutokana na kuwa ndiyo zao pekee la kiuchumi linatotegemewa na wananchi wa bonde hilo la songwe.
Waliongeza kuwa kwa sasa maisha yamekuwa magumu kutokana na kukosa fedha hizo na kwamba hawajui pa kuanzia katika kufanya maandalizi ya shamba na kuanza kupanda tumbaku kwa ajili ya msimu mwingine kutokana na kukosa pembejeo za kilimo.