TAWI LA CCM HUKO " UNITED KINGDOM" LAMPONGEZA DR.DALALY KAFUMU KWA USHINDI



CHAMA CHA MAPINDUZI.
TAWI LA UNITED KINGDOM.
2 Apple Shaw Court, School Rd, Reading, RG31 5AL.
Katibu wa Tawi  Direct Tel.  +44 7799435327 or Email katibuwatawi@ccmlondonuk.org
Mwenyekiti wa Tawi  Direct Tel +44 7900040288. Or Email  owinoz@yahoo.co.uk
Website: www.ccmlondonuk.org  E-mail: ccmlondon@gmail.com


PONGEZI KWA DR. KAFUMU DALALY KWA KUSHINDA UBUNGE KATIKA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA IGUNGA: TAREHE 02/10/2011.

Wana Chama Cha Mapinduzi Tawi la United Kingdom tunatuma salaam za pongezi za dhati kwa Dr. Peter Kafumu Dalaly kwa kuzitetea Sera na Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 na hatimaye kushinda nafasi ya ubunge katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Igunga uliofanyika  tarehe 02 Oktoba, 2011.
Aidha tunawapongeza wana Igunga wote kwa kufanya Uamuzi na Uchaguzi wa   Busara kwa kuichagua CCM na Dr. Dalaly. Tunawashukuru viongozi na wana CCM waliojituma kuhakikisha Ushindi unapatikana. Wana Igunga wamethibitisha kuwa Uongozi na Uwakilishi Bora unatoka ndani ya CCM. Tunaungana nao kukukumbusha, Dr. Dalaly, kuwa tofauti ya KURA za ushindi ni ndogo na wananchi  ambao hawakupiga Kura ni wengi, hivyo basi hii ni changamoto kwetu kwamba ni lazima CCM tuendelee kujisahihisha kwa kuwasikiliza wananchi na kutatua KERO zao kwa kasi ya ziada kwa kuwa wengi bado wana imani na Chama Cha Mapinduzi.
Ni wajibu wetu kukumbushana kuwa zoezi hili la demokrasia ya uchaguzi mdogo jimboni Igunga limeigharimu Taifa letu maskini fedha taslimu na rasilimali nyingi na wakati muhimu. Kwa kuwa wana Igunga wameidhamini CCM pamoja nawe ridhaa ya uwakilishi, basi  ni vema:-
1. Uwalipe wana Igunga haki yao kwa kuandaa ratiba mahsusi ya kuwatembelea katika vitongoji vyao na kuandaa mkakati madhubuti utakao chochea ubunifu wa kujiajiri ili kuzalisha na kuvuna raslimali mpya za Taifa ili kuleta maendeleo jimboni.
 2. Uwe mwakilishi mahiri na mshauri makini ndani ya Bunge ili Serikali na wadau wote wa maendeleo ya kitaifa wanufaike na mchango wako mpya wa mawazo.
3. Uwe chachu mpya itakayowezesha Serikali na Asasi binafsi kuweza kushirikiana kwa pamoja ili kuwafuata wananchi na kuwatengenezea mazingira yenye kuamsha vichocheo vya miradi ya maendeleo mkoani Tabora.
CCM UK tunakutakia kheri njema katika majukumu yaliyo mbele yako tukiamini kwamba utaushirikisha utashi wako, maadili ya uongozi na fikra tendaji katika kukishauri Chama, Serikali na Umma kupitia Vikao vyote halali ili kuongeza kasi ya maendeleo.

TUMEAHIDI,  LAZIMA TUTEKELEZE.
Imetolewa na: CHAMA CHA MAPINDUZI -(UK)
          LONDON, UNITED KINGDOM.
          03 Octoba, 2011

Posted by Bigie on 5:27 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.