WAPIGA NONDO WALIO MUUA ASKARI POLISI WA MBEYA WAFIKISHWA MAHAKAMANI


WASHTAKIWA watatu wanaotuhumiwa kwa mauaji ya askari polisi G 2795 PC Urasa wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya jana na kusomewa shtaka la mauaji ya kukusudia.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi, Zawadi Laizer, Mwanasheria wa Serikali Basilius Namkambe alisema washtakiwa Edson Olendo (28), Rashind Mwakangwe (30) na Erasto Elias maarufu kama Mzazi (30) wakazi wa Inyara wilaya ya Mbeya wote kwa pamoja wanashtakiwa kwa kosa la mauaji ya kukusudia kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 196 cha makosa ya jinai.

Alisema washtakiwa hao kwa pamoja mnamo Septemba 26, mwaka huu, katika eneo la Mabatini jijini hapa walimuua kwa kukusudia askari polisi mwenye namba G 2795, PC Urasa.
Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote mahakamani hapo na ndipo Hakimu Laizer aliamuru washtakiwa kupelekwa rumande hadi Oktoba, 24 siku ambayo kesi yao itatajwa kwa mara ya kwanza katika mahakama kuu.

Askari huyo aliuawa Septemba 27 mwaka huu na kuagwa Septemba 28 ambapo mkuu wa wilaya ya Mbeya Evance Balama na kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi waliongoza wananchi na askari katika kuuaga mwili wa marehemu.

Posted by Bigie on 8:39 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.