NELLY KAMWELU AINGIA 5 BORA KATIKA SHINDANO LA MISS TOURISM QUEEN INTERNATIONAL 2011/2012
JAMII 11:12 PM

Nelly Kamwelu ambaye ni mshindi wa Miss Universe Tanzania 2011 (wa kwanza kushoto)ameingia  katika 5 bora ya mashindano ya utalii ya Miss Tourism Queen  International 2011/12 yaliyofanyika nchini China mji wa Xian. 
Nelly  ameshika nafasi hiyo mbele ya warembo wengine 92 katika shindano hili  ambalo ni la 5 kwa ukubwa duniani. 
Mshindi wa taji la Miss Tourism Queen  International alikuwa Mrembo wa Thailand, mrembo wa Fernando de Noronha  alishika nafasi ya pili, Belarus nafasi ya tatu na mrembo wa China  ashika nafasi ya 4.    Nelly anarejea nchini tarehe 29 na ndege na  Emirates.





