MKUU WA WILAYA YA KOROGWE AKARIBISHA WAWEKEZAJI WENYE NIA YA KUJENGA HOTELI KUBWA WILAYANI HUMO
JAMII 11:12 PM
Mkuu  wa wilaya ya Korogwe Bw. Erasto Sima, akiweka jiwe la msingi katika  MGAHAWA wa Rock Hill Rest uliopo katika barabara kuu ya Korogwe/Same  katika kijiji cha Kiloza ambao ni maalumu kwa ajili ya wasafiri  wanaotumia barabara ya Kasakazini yenye mikoa ya Tanga, Kilimanjaro,  Arusha na Manyara.
Mkuu  wa wilaya ya Korogwe Bw. Erasto Sima, akizungumza katika uwekaji wa  jiwe la msingi katika MGAHAWA wa Rock Hill Rest mara baada ya kuweka  jiwe hilo la msingi, anayefuata baada ya Mkuu wa wilaya ni Mkurugenzi wa  Mgahawa huo Bw. Estomio Urio na wengine ni wajumbe wa kamati ya ulinzi  na usalama wa wilaya ya Korogwe.
Wafanyakazi  na wadau wakubwa wa mtandao huu, wakiwa wameandaa chakula tayari kwa  wateja wao watakaofika hapo iwe ni kwa mabasi makubwa au magari madogo.
Eneo  la mgahawa wenyewe unavyoonekana ukiwa chini ya mlima wa Lutindi ambao  umekuwa ukileta upepo kwa wasafiri wanaofika kupata chakula katika  mgahawa huo.
Katika  uwekaji wa jiwe hilo la msingi Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bw. Erasto  Sima aliendelea kuita wawakezaji katika wilaya hiyo ambao wataweka  migahawa mikubwa na hoteli katika wilaya hiyo kwa lengo la kusaidia  kutoa ajira na pia ulipaji wa kodi kwa serikali.
Alisema  suala la uwekezaji kama huo ni muhimu lakini pia aliwaasa wawekezaji  wanaowekeza miradi mikubwa kama hiyo kuishi vizuri na wananchi  wanaozunguka maeneo hayo ikiwemo kusaidia huduma za jamii katika eneo  hilo badala ya wawekezaji kuzalisha migogoro.
Mmiliki  wa mgahawa huo mzuri Bw. Urio alisema anaishukuru benki ya CRDB kwa  kumwezesha kumpatia mkopo ambao umemfanya aweze kujenga mgahawa huo  katika kipindi cha mwaka mmoja kwa gharama ya shilingi milioni 800 hadi  sasa ukiwa umefikia awamu ya kwanza ambapo anatarajia kujenga hoteli na  kuimalizia katika awamu ya pili anapotarajia kutumia shilingi bilioni  1,6 hadi kukamilisha mradi wake huo.
Mgahawa  huo wa chakula kwa wasafiri kwa barabara hiyo unakuwa ni wa Nne mkubwa  baada ya ule wa Liverpool uliopo eneo la Mombo, Mombo Resort, Dar  Express (Highway Resort) na huu sasa Rock Hill Rest.





