JACKLINE WOLPER HUENDA AKAFUNGIWA KUCHEZA FILAM KWA KIPINDI CHA MIEZI KUMI
JAMII 9:55 PM
MSANII nyota wa bongo movie Jackline Wolper, huenda akafungiwa kucheza filamu kwa miezi 10 na Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, kwa kilichodaiwa kuwa mwaka uliopita alitoa kauli za kulichafua shirikisho hilo.
Habari za siri zilizopatikana kutoka ndani ya shirikisho hilo, zinasema kuwa msanii huyo alitoa kauli za kuwagawanya wasanii huku akidai kuwa Rais wa shirikisho hilo anafanya kazi bila kuwashirikisha wasanii.
Chanzo cha habari kilichozungumza na Mpekuzi wetu, kilisema kuwa kuna vikao cha siri ambavyo vinamjandili msanii huyo lakini watu wengi wanaonekana kutoa kauli za kutaka msanii huyo aafungiwe kwa miezi hiyo 10.
Hata hivyo mpekuzi wetu alimtafuta Wolper ili kujua kama ukweli wa habari huo ambapo alisema kuwa hakuna ukweli wowote juu ya hilo. Alidai kuwa kuna kundi la watu ambalo linataka kumweka mbali na tasnia.






