DIAMOND ATAKIWA KUTINGA "MAHAKAMANI" KESHO SAA MBILI ASUBUHI


NYOTA wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, Jumatatu atapanda kwenye kizimba cha Mahakama ya Wilaya, Iringa akikabiliwa na msala wa kuharibu mali.
 
Kwa mujibu wa chanzo chetu, msanii huyo anatakiwa kutinga mahakamani hapo asubuhi ya saa 2:30, bila kukosa huku ikisemekana mlalamikaji alilazimika kufungua kesi hiyo kufuatia mlalamikiwa kupuuza makubaliano.

Diamond ambaye yumo ndani ya mgogoro mkubwa na aliyekuwa mchumba’ake, Wema Sepetu, alishikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Iringa siku moja kabla ya kuingia kwa mwaka mpya wa 2012 akidaiwa kuharibu mali ya mwandishi wa habari, Francis Godwin.

Katika sakata hilo, Diamond alitakiwa kumlipa mwandishi huyo Sh. milioni 1.8 na kumuomba msahama yaishe.

Hata hivyo, taarifa zilidai kuwa mwandishi huyo alichomoa kulipwa na kudai kuwa anataka ampe "shule"

Posted by Bigie on 10:12 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.