KAJALA AHITAJI MILIONI 50 ILI KUFANIKISHA UJIO WA FILAM YAKE MPYA


MSANII wa filamu bongo, Kajala, ameripotiwa akisema kuwa anahitaji zaidi ya shilingi milioni 50, kwa ajili ya kuandaa filamu yake mpya ambayo itakuwa na nyota kutoka nje.

Akizungumza na
mpekuzi wetu, nyota huyu alisema  kiasi hicho cha pesa anahitaji kukipata ifikapo Julai mwaka huu kwani mchakato wa kuandaa filamu hiyo unatarajia kuanza Agosti mwaka huu.

Alisema jina la filamu hiyo bado gumu pamoja na wasanii kutoka nje ambapo watajulikana baada ya mchakato mzima wa mazungumzo, ingawa wanatarajia kutoka
Ghana, Nigeria na Kenya.

Aliongeza kuwa kwa upande wa nyota wa bongo atawatumia wale ambao hawana majina makubwa kwa lengo la kuwatoa zaidi kimataifa.


“Najua hii ni kazi hivyo nahitaji kiasi hicho cha pesa ili niweze kutimiza ndoto zangu, ambapo naamini endapo pesa hizo zitapatikana basi kila kitu kitakuwa sawa,”
alisema.

Hata hivyo
mpekuzi wetu,alitaka kujua atatumia njia gani ili kuweza kupata pesa hizo, ambapo alisema kuwa anajitahidi kuzungumza na kampuni mbalimbali ili ziweze kumkopesha kiasi chochote cha fedha.

Posted by Bigie on 9:29 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.