ROSE NDAUKA AINADI FILAM YAKE MPYA YA "LOVE ME"


MWANADADA kipenzi cha mashabiki ndani ya bongo movie Rose Ndauka , amesema kuwa anatarajia kuachia filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Love Me’.

Ndauka akizungumza na
mpekuzi wetu, alisema kuwa filamu hiyo itaonesha muonekano mpya wa Afrika ambapo hakutakuwa na matukio ambayo yanaweza kuchafua maadili.

Alisema kuwa filamu hiyo itaonesha matukio mengi kama vile mapenzi, usaliti na matukio mengine mengi ambayo yatakua ni fundisho kwa jamii.


“Nipo katika mchakato wa kuitoa filamu yangu iitwayo  ’Love Me’, ambayo itakuwa ya kiafrika zaidi kwani watu wengine wamezoea kusema kwamba filamu zetu tunacheza kama wazungu hivyo sasa wategemee ujio tofauti kabisa,”
alisema.

Sambamba na hilo msanii huyo aliwaomba mashabiki wake kuitafuta filamu hiyo pindi itakapokuwa sokoni kwani itaonyesha maisha halisi ya mapenzi na matukio mengine mengi ya kusisimua.

Posted by Bigie on 9:25 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.