KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII YAFANYA ZIARA JIJINI MWANZA


Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt Faustin Ndungulile (aliyevaa shati la kitenge karibu na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo, wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa mkoa huyo wakijitambulisha kuhusu kufanya ziara ya siku tatu mkoani humo kutembelea sekta ya afya.
Mwenyekiti wa Bodi ya Bohari Kuu ya Madawa nchini (MSD) Bi Eva Nzaro (wa kwanza kulia) akiwa na mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii, Dkt Ndungulile (mwenye shati la kitenge) akimuongoza pamoja na wajumbe wengine wa kamati hiyo kwenda kutembelea bohari ya kuhifadhia dawa ya Kanda ya Ziwa iliyopo Jijini Mwanza.
Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii wakiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wao Dkt Ndugulile, wakimsikiliza Mkurugenzi wa kanda ya ziwa wa MSD akitoa maelezo namna wanavyoweza kuhifadhi dawa kisha kuzisambaza kwa wateja wao mbalimbali wa mikoa ya Mwanza, Musoma, Bukoba, Shinyanga na mkoa mpya wa Geita.
Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijiji mkoani Tanga (CCM) Stephen Ngonyani 'almaarufu Profesa Majimarefu' ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Huduma za jamii, akimsalimia mgonjwa Josephine Kalekwa aliyelazwa katika kituo cha afya cha Sangabuye kilichopo katika kata ya Sangabuye, wilayani Ilemela. Mwingine ni Mbunge wa Biharamulo Dkt Antony Mbasa (Chadema), wakati kamati hiyo ilipofika katika kituo hicho cha afya kuangalia matatizo mbalimbali.
Pamoja na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng. Ndikilo kulalamika kwamba kuna uhaba mkubwa wa dawa katika hospitali nyingi mkoani humo licha ya MSD kuwasilishiwa fedha lakini wajumbe wa kamati hiyo walishuhudia shehena na mabox ya dawa yakiwa yamehifadhiwa kwenye bohari hiyo ya madawa kanda ya ziwa

Posted by Bigie on 8:38 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.