MRADI WA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA VVU/UKIMWI ULIOFADHILIWA NA SERIKALI YA JAPAN WAFUNGWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM

Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akimkabidhi Zawadi iliyoandaliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mwakilishi mkuu wa JICA wakati wa hafla fupi ya ukamilishaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini uliofadhiliwa na serikali ya Japan jijini Dar es salaam.
Mwakilishi mkuu wa Shirika la Kimataifa la ushirikiano wa kimaendeleo la Japan (JICA) Bw. Yukihinde Katsuta akitoa maelezo juu ya ukamilishwaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini Tanzania uliofadhiliwa na serikali ya Japan kwa lengo la kupunguza maambukizi ya VVU sanjari na usambazaji wa vifaa vya kupimia maambukizi hayo na kuahidi kuendeleza ushirikiano na serikali ya Tanzania katika utoaji wa vifaa vya kutolea huduma za afya.
Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akizungumza watendaji wa Wizara hiyo na wawakilishi wa Shirika la Kimataifa la ushirikiano wa kimaendeleo la Japan (JICA) wakati wa hafla fupi ya ukamilishaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini ulioanza mwaka 2009 chini ya ufaufadhili wa serikali ya Japan, jijini Dar es salaam.
Baadhi ya watendaji wa wizara ya afya na wawakili kutoka Shirika la kimataifa la maendeleo la Japan (JICA) wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zinatolewa wakati wa hafla fupi ya ukamilishaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini uliofadhiliwa na serikali ya Japan jijini Dar es salaam

Posted by Bigie on 8:35 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.