"SIKUPATA KITU NIKIWA NA DIAMOND ZAIDI YA NUKSI,NAOMBA ANIACHE...."WEMA SEPETU


STAA mwenye nyota ya kukubalika Bongo, amemtuhumu  vibaya aliyekuwa mchumba wake, Naseeb Abdul ‘Diamond’ kuwa ana nuksi.

Wema aliye Miss Tanzania mwaka 2006 na msanii anayetingisha kwenye soko la filamu za Kibongo kwa sasa, alisema hayo mara baada ya kutoka kwa habari katika gazeti moja linalotoka mara mbili kwa wiki, ikidai bado anamng’ang’ania Diamond.

Katika habari hiyo, Diamond anamtuhumu Wema kuendelea kumganda na kwamba alimfuata nyumbani kwake Sinza Mori, jirani na Baa ya Meeda alipohamia hivi karibuni, kwa lengo la kujaribu kutafuta suluhu.

Akizungumza na mpekuzi wetu kwa njia ya simu, juzi Jumatatu, Wema alisema hana mpango tena na Diamond kama alivyodai kwenye gazeti hilo.

“Sifikirii kuwa naye, halafu mimi ndiye niliyemtema...kwa nini nimhangaikie? Anataka kutafuta umaarufu kupitia jina langu. Kwa nini asifanye mambo yake?

“Sijazoea kujibizana kwenye magazeti, kama anataka kusema, aendelee lakini mimi sipo tayari kwa malumbano. Halafu namshangaa sana, kwa nini anamwingiza mama yangu kwenye haya mambo yasiyomhusu?” alifoka Wema.

Alisema, alichokiongea Diamond ni ‘utumbo’ tu na hakuna cha maana kilichomwingia akilini, zaidi ya kumuona kama mfa maji anayetapatapa.

Akienda mbali zaidi, Wema alifunguka kuwa kwa kipindi alichokuwa na Diamond, dili zake nyingi zilikuwa haziendi poa lakini muda mfupi baada ya kuachana naye, kila kitu kinakwenda sawa.

Kwa kauli hiyo, Wema anaonekana kumaanisha kuwa Diamond ana nuksi, ndiyo maana baada ya kutemana naye anakula kuku kwa mrija.

Alisema: “Sikupata kitu nikiwa na Diamond zaidi ya nuksi... tangu nimeachana naye naona mambo yangu yananyooka. Naomba aniache nipange maisha yangu...

“Nipo happy kuliko nilivyokuwa naye, mambo yangu yanakwenda sawa zaidi kuliko mwanzo, sitaki kusikia habari zake. Sitaki kurudia mambo ya zamani ambayo kwangu mimi hayana maana.

“Sasa hivi naishi maisha mapya, nina mipango yangu na inakwenda vizuri, huyo Diamond ni nani kwangu? Sitaki kumsikia kabisa. Nina kazi nyingi za kufanya, siyo kulumbana naye na kufaidisha watu.” 

Akaongeza: “Diamond ameshajua nina nyota nzuri, sasa asinitumie kujipandisha chati. Sitaki anishirikishe kwenye mambo yake na nimeshaamua kwamba sitaki kuwa naye, hata yeye anajua. Awe mkweli.”
 Wema alitoa onyo kali kwa Diamond, akimtaka aache kumfuatafuta kwa kuwa kwa sasa kila mtu ana maisha yake.
“Diamond anatakiwa kufahamu kwamba nimeshaachana naye. Basi aniache...Diamond aniache...aniache 
Diamond...sitaki tena kumsikia. Aniache please,” alisema.

Posted by Bigie on 4:47 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.