LULU MICHAEL ANASWA "AKIDENDEKA" NA MSANII MWEZAKE WA KIKE


ELIZABETH Michael ‘Lulu’ amesahau waraka alioandika Mwaka Mpya 2012 kuwa amejirekebisha na hataki tena skendo kwani kabla ya mwezi Januari kumalizika, tayari amekwaa skendo namba moja ya kujihusisha na vitendo vya kisagaji.

Picha ya Lulu anayefanya poa kwenye filamu za Kibongo imenaswa mtandaoni akilishana keki kwa staili ya ‘kudendeka’ na msanii anayeuza nyago kwenye video za wanamuziki wa Bongo Fleva, Halima Mohamed ‘Baby Candy’.
Picha hiyo ilionesha ilipigwa ndani Club Bilicanas, Dar es Salaam, Jumapili ya Januari 15, mwaka huu.


Tukio hilo limesababisha mjadala mzito kwa watu walioiona picha hiyo kwenye mtandao wa BBM kufuatia kuwepo kwa tuhuma zinazoenea kwamba baadhi ya mastaa wa filamu kwa sasa wamejikita zaidi kwenye mchezo huo.

“Inawezekana ni mtindo wa kisasa kulishana keki kwa mdomo, lakini hawa wamezidisha hasa katika kipindi hiki ambacho wasanii wengi wanatuhumiwa kujihusisha na usagaji,” ilisomeka sehemu ya maoni ya picha hiyo.


Baada ya kuona mjadala unazidi kushika kasi, mpekuzi wetu alimtafuta Lulu ili kupata undani wa picha hiyo ambapo hakuonesha kushtushwa na chochote kwa kudai ni jambo la kawaida.

“Ni kweli ilikuwa Bilicanas, siku hiyo shosti wangu Baby Candy alikuwa na sherehe ya kuzaliwa, kwangu mimi hakuna ubaya wowote,” alifunguka Lulu nusunusu kwa kukataa maswali zaidi.

Posted by Bigie on 3:29 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.