PICHA MPYA ZA WEMA NA KANUMBA ZAZUA MASWALI MENGI
JAMII 3:37 PM
PICHA mpya za pamoja walizopiga Wema Isaac Sepetu na Steven Charles Kanumba, zimezua gumzo jipya na watu wanahoji imekuwaje tena wakati ‘wanasemaga’ hawana ukaribu wowote?
Wema aliziweka picha hizo kwenye mtandao wa BlackBerry Messenger (BBM) juzikati ili kuona kama watu watasemaje ambapo ndani ya dakika chache, alikuwa ameshambuliwa vibaya kwa maoni kibao.
Katika tukio hilo lililojiri Januari 17, mwaka huu, Wema alilazimika kuiondoa picha hiyo mara moja kwani watu walikuwa wakitaka kujua ukaribu huo ulitokana na mazingira gani.
Hata hivyo, mpekuzi wetu alipozungumza na Wema juu ya ishu hiyo, alisema kuwa alikutana na Kanumba kwenye mahojiano katika Runinga ya EATV, ndipo wakapiga picha hizo.
“Sipendi bifu na mwanaume niliyeachana naye, nikimwagana na mtu, haina maana kwamba hatuwezi kushea, picha tulipiga watu wengi na wala hazimaanishi nimerudiana na Kanumba,” alisema Wema aliyewahi kuwa mpenzi wa staa huyo wa muvi za Kibongo.






