MTU ASIYEFAHAMIKA ATUMIA JINA LA ROSE NDAUKA KUTAPELI 200,000/=
JAMII 11:52 PM
NYOTA wa sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka amejikuta akibeba tuhuma nzito kufuatia mtu asiyejulikana kutumia jina la msanii huyo kuomba fedha kwa profesa mmoja wa Chuo Kikuu kimoja maarufu Dar
Habari zinadai kuwa, Rose Ndauka huyo feki alipata namba ya simu ya profesa huyo na kuanza mawasiliano naye kisha akafikia hatua ya kumwomba shilingi 200,000 akidai ana matatizo.
“Kilichomshangaza profesa ni kitu kimoja, kila alipokuwa akimpigia simu huyo Rose, alikuwa hapokei, lakini akituma meseji anajibiwa vizuri, akashtuka.
“Sasa kuna siku profesa alikutana na msanii mwingine wa filamu, Riyama Ally na kumsimulia, ikabidi Riyama ampigie Rose ambaye alikataa kuomba fedha kwa profesa huyo.
“Lakini Riyama pia alipoiangalia namba ya simu ya Rose kwa profesa na ile aliyonayo yeye zilikuwa tofauti, akamwambia profesa take care, unaibiwa,” kilisema chanzo hicho.
Juzi jumanne, Rose alikiri kutokea kwa sakata hilo na kusema kuwa kuna watu walioibuka ambao wanatumia majina ya mastaa kutapeli.
“Kwani unadhani siri, niliambiwa hizo habari na Riyama, nikashangaa sana. Halafu si mimi tu. Halafu hao matapeli hata siku moja hawapokei simu, wao ni meseji tu,” alisema Rose.






