MR. NICE NA REHEMA FABIAN WANASWA LIVE
JAMII 12:00 AM
MFALME wa mtindo wa muziki wa Takeu Bongo, Nice Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’ amenaswa laivu akidendeka kimahaba na Mshiriki wa Miss Kiswahili 2008, Rehema Fabian.
Wawili hao walinaswa mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Meeda, Sinza Mori jijini Dar es Salaam ambapo Bendi ya Extra Bongo na msanii wa Bongo Fleva, Khalid Ramadhan ‘Tundaman’ walikuwa wakikamua.
Mwanzoni wapenzi hao walishudiwa wakiingia ukumbini humo kwa staili ya kujinafasi na kwenda kaunta huku wakiwa sanjari na msichana mmoja ambaye jina lake halikujulikana.
Wakiwa kaunta wakikata kilaji, Mr. Nice alimuomba Rehema wakacheze ambapo mrembo huyo alionesha dalili za kugoma, kitendo kilichomfanya staa huyo kumbeba kwa nguvu.
Rehema alikubali kucheza lakini cha ajabu Mr. Nice badala ya kuunga mkono kucheza yeye akaanza kumla denda bila kujali watu waliokuwa wakiwakodolea macho, Rehema naye akaunga mkono hali hiyo.
Source: GPL






