NISHA AMTUHUMU REHEMA FABIAN KUWA NDIYE ALIYETOROKA NA MCHUMBA WAKE


MREMBO anayetesa kwenye kiwanda cha filamu bongo Salma Jabu ‘Nisha’, ametapika maneno na kutoa siri iliyovuruga ndoa yake ambapo anadai kuwa Rehema Fabian, ni mwanamke ambaye alitoroka na mpenzi wake mwezi mmoja wakati wakikalibia kufunga ndoa.

Nisha
alitangaza kufunga ndoa mwaka jana lakini hali haikuwa kama alivyopaga, baada ya Rehema kudaiwa kumchukua mchumba wa Nisha na kutoraka naye hadi Zanzibar walikoenda kula bata.

Akitapika maneno hayo
Nisha, alisema kuwa awali hakujua nani alimchukua mchumba wake lakini baada ya rafiki zake wa karibu na Rehema, ndiyo waliyompasha ukweli juu ya tukio hilo kusisimua.

Alisema kuwa baada ya kujua ukweli huo alifanya uchunguzi wake wa kufutilia sehemu walipo ambapo aliwakuta Visiwani Zanzibar walikila bata.
“Mimi kwetu ni Zanzibar hivyo hakuna sehemu ambayo siijui hivyo nilifanya uchunguzi wangu hadi nikajua sehemu ambayo walikuwa wanafanyia ujinga wao,” alisema.

Nisha alisema baada ya kushuhudia kwa macho yake aliamua kuachana nao ingawa alikuwa anampenda sana mchumba wake ambaye ametengana naye kwa sababu ya utapeli wa
Rehema.

Baada ya
mpekuzi wetu kupata maneno kutoka upande wa Nisha, iliamua kumtafuta Rehema, naye alisema kuwa habari hizo hazina ukweli wowote ha hakuwahi kumuibia mchumba wake tangu aanze kujuana naye.

Alisema hata yeye alisikia habari hizo kuwa analalamika kuwa ameibiwa mpenzi wake lakini kwa upande wake haoni kama yeye anahusika na tukio hilo.


“Nasema ukweli wangu sijawahi kutoka na mpenzi wa Nisha, kwani ni rafiki yangu hivyo naheshimu mapenzi ya watu ingawa yeye anasema hivyo,”
aliongeza.

Posted by Bigie on 1:20 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.