REHEMA FABIAN ATUHUMIWA KUMTOROSHA DOGO JANJA


MSHINDI wa shindano la kumsaka Balozi wa Kiswahili Bongo mwaka 2009, Rehema Fabian (pichani), anadaiwa kwenda Manzese, Dar anakoishi msanii Abdulaziz Abubakar Chende ‘Dogo Janja’ na kumtorosha

Akifunguka juzikati jijini Dar, mlezi wa Dogo Janja ambaye pia ni Rais wa Manzese na Kundi la Tip Top Connection, Hamad Ally ‘Madee’ alisema Rehema alifanya kosa hilo hivi karibuni na kwamba limemsikitisha sana.

Alisema siku ya tukio, alirudi nyumbani saa tisa usiku na kumkosa msanii huyo, alipouliza akajibiwa alifuatwa na demu mmoja ambaye mara nyingi huwa beneti na Tundaman (Rashid Ramadhan).

Madee alisema kuwa alipomuuliza Tundaman ni demu gani huwa naye beneti mara nyingi, alimjibu kuwa ni Rehema Fabian.

“Aliponiambia hivyo nilianza kuwasaka, nikasikia wapo viwanja, sijui wapi huko! Niliingia mtaani kuwatafuta lakini sikuwaona,” alisema Madee.

Aliongeza kuwa kibaya zaidi, yeye ndiye aliyekabidhiwa dogo huyo kutoka kwa wazazi wake, Arusha.

“Mimi ndiye niliyekabidhiwa Dogo Janja, nakaa naye, lolote litakalomtokea nitaulizwa mimi,” alisema.

Akaongeza: “Sasa kwa mfano katika safari yao wangepata ajali, nani angeulizwa? Halafu mlango waliuacha wazi. Kwa kweli siwezi kumvumilia, nitahakikisha namfunza adabu (Dogo Janja), nikishindwa namrudisha kwao Arusha.”

Kwa upande wake, Rehema alisema si kweli kuwa alimtorosha Dogo Janja, bali anachokumbuka  dogo huyo alimpigia simu akimtaka ampe ofa ya kwenda kumlipia kwenye ‘swimming pool’ ili aogelee.

“Lakini kwa vile nilikuwa bize sikumfuata, nashangaa kutuhumiwa eti nilikwenda kumtorosha,” alisema Rehema.

Akasema: “Unajua Dogo Janja ana mambo makubwa, inawezekana kuna mwanamke mwingine alikwenda kumtorosha alipobanwa akanitaja mimi. Mimi nikimtaka nitamuomba Madee lakini siwezi kumtorosha, labda kuna mengine yamejificha.”

Posted by Bigie on 1:31 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.