NORA ATAKA "NDOA ZA MIKATABA"...ADAI KUWA AMECHOKA KUISHI NA MWANAUME KWA MUDA MREFU
JAMII 5:07 PM
NYOTA aliyewahi kutamba katika kundi la sanaa la Kaole,Nora, amesema kikubwa anachotaka sasa ni kufunga ndoa kwa mkataba, kwani amechoka kuishi na mwanaume kwa muda mrefu.
Msanii huyo ni mke wa mtu lakini anaonekana kutoifurahia ndoa yake kutokana hamu hiyo ya kutaka kuolewa kwa mkataba.
Akiwa katika mazungumzo na mpekuzi wetu,ambaye ni rafiki yake waa karibu,Nora alisema kuwa mume wake amekuwa akimkataza asijihusishe na sanaa kwa madai kuwa ndani ya tasnia hiyo kumejaa uhuni kitu ambacho haoni kama kina ukweli wowote juu yake.
“Napenda kuishi na mume lakini kwa mkataba kwani sitaki kuishi nikiwa chini ya mtu kitu ambacho kinanifanya nishindwe kufanya mambo yangu mengine,” alisema Nora
Nora aliongeza kuwa katika mkataba huo hataki kuzaa na mtu kwani haitaji kuwa na watoto wengi ambao watakua na baba tofauti.