JE,NI KWELI BABY MADAHA ALITAPELI KIASI CHA 500,000/= ?
JAMII 5:07 PM
MATATIZO yanaendelea kumkabili msanii wa filamu bongo,Baby Madaha , baada ya sasa kufikishwa kituo cha polisi cha Oysterbay kwa madai ya utapeli wa shilingi laki 500,000, kutoka kwa kampuni moja inayohusika na masuala ya urembo ambapo juzi alitolewa kwa dhamana na familia yake.
Awali nyota huyo alidaiwa kuwatapeli wasanii chipukizi kiasi cha shilingi laki 300,000, ingawa hawakuweza kumfikisha popote.
Chanzo cha habari cha kuaminika kilichozungumza na mtandao huu, kilisema kuwa msanii huyo alikopa kiasi hicho cha fedha kwa madai kuwa rafiki yake wa karibu anaumwa hivyo alihitaji kiasi hicho ili ziweze kumsaidia katika matibabu.
Kilisema kuwa baada ya kukopa fedha hizo aliamua kutoroka jijini na kwenda kuishi Morogoro, kitu ambacho kiliwapa mashaka watu ambao walimkopesha fedha hizo na kwenda kutoka taarifa kituo cha polisi.
“Siwezi kusema kama ni kweli alikuwa na nia ya kutapeli lakini kwanini baada ya kupewa fedha hizo aliamua kwenda kuishi Morogoro, wakati makazi yake yapo hapa jijini tena baada ya kupewa fedha hizo tu,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Baada kupata ishu hiyo Baby Madaha alitafutwa ili kujua undani wa habari hiyo lakini baada ya kupatikana alionekana kujibu kwa wasiwasi,ishara ambayo ilidhihirisha wazi kuwa kulikuwa na kitu nyuma ya pazia

Baada ya maswali kadhaa aliamua kufunguka na kusema kuwa hajatapeli fedha hizo na alienda Morogoro kwa matatizo yake, lakini habari za kufikishwa polisi hazina ukweli kwani alienda kituo cha polisi kwa ajili ya mazungumzo rafiki na mmoja wa askari wa kituo hicho.
“Hizo habari hazina ukweli kwani sina tabia ya kutapeli ingawa fedha hizo nilichukua, pia nilienda pale polisi kwa kazi zangu si kwamba niliwekwa ndani,” alisema.