ROSE NDAUKA AJIWEKA MBALI NA "MAKUNDI NDANI YA BONGO MOVIES"
JAMII 5:22 AM
MREMBO ndani ya bongo movie Rose Ndauka, amesema kuwa mwaka huu haitaji kujihusisha na makundi ya wasanii kwani ndiyo yanayokuwa chanzo cha matatizo katika tasnia hiyo.
Awali msanii huyo alikuwa na urafiki wa karibu na Wema Sepetu na Jackline Wolper , lakini kutokana na matatizo fulani urafiki wao umekuwa wakusuasua.
Ndauka alisema kuwa mwaka uliopita makundi hayo ndiyo yaliyomponza na kujikuta katika matatizo kwani baadhi ya wasanii hawapendi mtu afanye kitu kizuri.
Aliongeza kuwa makundi hayo yamekuwa na tabia ya kuchukuliana wanaume huku wakitangaza maneno mabaya kwenye vyombo vya habari.
“Mimi sitaki kujihusisha na makundi ambayo hayana faida kwangu kwani baadhi ya wasanii ambao utakuwa nao karibu wanakuwa wa kwanza kukuchukulia wanaume na mwisho wa siku wanajisifia kuwa yule hana lolote kwanza hata mpenzi wake tumemchukua,” alisema.
Aliongeza kama kuna msanii anahitaji kuwa naye kwa sasa basi lazima amchunguze tabia zake ili yasije yakamkuta kama ya mwaka jana.