SALMA JABU (NISHA) AAMUA KUACHANA NA POMBE NA SIGARA
JAMII 2:37 AM
MWANADADA anayefanya vizuri kunako tasnia ya filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amesema kuwa ameamua kuachana na uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe baada ya kumpata mpenzi anayemjali.
Nisha alimwambia mpekuzi wetu hivi karibuni kuwa, kipindi cha nyuma kidogo alikuwa amekubuhu kwenye ulevi kutokana na kuteswa na mapenzi lakini sasa anaachana na anasa hiyo.
“Mwaka huu nimeanza vizuri, naacha pombe na sigara baada ya kumpata mwanaume anayenipenda kwa dhati na kunijali kwa kila hali,” alisema Nisha.
Aidha, msanii huyo alisema kuwa atahakikisha anaepukana na tabia zisizofaa ili kumshawishi mpenzi wake huyo wafikie hatua ya kuoana kabla ya kuisha mwaka huu.






