SHILOLE APATA MCHUMBA WA KITANGA...


MSANII mrembo wa tasnia ya filamu bongo, Zena Muhamed ‘Shilole, amesema anajisikia ni mtu mwenye furaha kwani amechumbiwa na mwanaume mmoja ambaye ni mfanyabiasha wa mafuta kutoka mkoani Tanga.

Msanii huyu kwa muda mrefu amekuwa akitafuta mwanaume wa kumuoa ambapo sasa anaonekana kuwa na furaha kwani ndoto yake ya imetimia.


Shilole alisema kuwa ndoa yake itafungwa muda wowote baada ya maandalizi yote kukamilika ambapo inaweza kufungwa mwezi Octoba mwaka huu. Hata hivyo aliongeza kuwa ndoa hiyo itafungwa kimila na si kama watu walivyozoea kufunga zile za kifahari.

“Yani naweza kusema kuwa mwaka huu utakuwa wa furaha sana katika maisha yangu, kwani nimepata mwanaume ambaye ndiye chaguo langu na kikubwa ni kwamba ndoa yetu tutafunga kimila,” alisema.

Posted by Bigie on 9:05 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.