SINTAH ATAMANI KURUDIANA NA "JUMA NATURE"


MUIGIZAJI nyota wa filamu Sintah, amesema mara nyingi amekuwa akiota ndoto za mapenzi akiwa na mpenzi wake wa zamani Juma Nature, kitu kinachomsukuma kutaka kurudiana naye tena.

Akizungumza na
Mpekuzi wetu, msanii huyo alisema hii ni wiki ya tatu tangu alipoanza kuota ndoto hizo ambazo zote humuonyesha vitu vyote walivyokuwa wanafanya walipokuwa wapenzi.

Alisema mara ya mwisho aliota wakiwa katika ufukwe wa bahari ya Hindi maeneo ya
Coco beach, lakini hadi hivi sasa hajui nini cha kufanya kwani  ndoto hizo zinamfanya ahisi bado anamapenzi mazito kwa msanii huyo.

“Yaani nashindwa kuelewa miaka yote sijawahi kuota ndoto kama hivi lakini baada ya kutangaza nataka kutoa filamu  yenye jina la wimbo la ‘Nature’ wa ‘Sitaki Demu’, basi hali imekuwa tofauti,”
alisema.

Hata hivyo msanii huyo alisema amekuwa akimpenda Nature, lakini kitu kinachomfanya awe mzito kumpa mapenzi ni kutokana na wimbo ulioimbwa na msanii huyo wa
Sitaki Demu’, ambao ulikuwa mahususi kwake.

“Nashindwa kuchukua maamuzi ya haraka kwani nikikumbuka wimbo ambao uliimbwa na Nature, kuhusu mimi basi hapo nakuwa mzito katika kufanya jambo ambalo linaweza kuwa na mafanikio hasa katika mapenzi”
aliongeza.

Sintah
na Nature walikuwa ni wapenzi miaki kadhaa iliyopita lakini walikuja kuachana baada ya Nature kusikia tetesi mbalimbali kuwa mrembo si mtu mzuri katika mapenzi yao.

Posted by Bigie on 4:34 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.