VAZI LA NUSU UCHI LAMTIA AIBU "MONALISA"
JAMII 9:15 AM
KIVAZI cha nusu uchi alichokuwa amevaa msanii wa filamu Bongo, Yvone Cherry Ngatwika ‘Monalisa’ kimemtia aibu mbele ya kadamnasi kutokana na kuanika sehemu zake nyeti.
Mona alinaswa ametinga kiwalo hicho hivi karibuni ndani ya Ukumbi wa New Maisha Club kulikokuwa na halfa iliyowakutanisha wasanii kibao.
Akiwa ukumbini hapo, mwanadada huyo ambaye ni mara chache sana huvaa mavazi ya dizaini hiyo alionekana amekaa huku akipata tabu kuficha maeneo yake muhimu bila mafanikio.
Baada ya kuona mambo yanaharibika, Mona aliamua kutumia pochi yake kujiziba lakini bado mapaja yake yaliyonawiri vilivyo yalibaki wazi hivyo kuibua minong’ono






