AUDIO TRACK: JOH MAKINI – MANUVA




Kuna wakati nimewahi kusikia “kaubishi” kuhusu nani wakali katika Hip Hop ya Bongo kati ya vijana wa Jiji la Dar-es-salaam na wale wa Jiji la Arusha.

Waliotetea lile kundi la A-Town wakasema kule ndipo penye Real Hip Hop kwa hiyo kimsingi “machalii” wa kule wapo juu zaidi.Wale wa Dar,huku wakitweta kwa hasira wakadai DSM ndipo chimbuko.

Ndipo walipoibukia makundi kama Kwanza Unit nk.Iweje useme A-Town ndipo panabamba zaidi?


Kinachochangia ubishi kama huo(hata kama hauna mantiki) ni pamoja na watu kama Joh Makini au Mwamba Wa Kaskazini kama anavyojulikana awapo kitaani na akiwa kwenye kazi. 

Ingawa kazi zake nyingi anazifanyia jijini Dar,inajulikana wazi kwamba anawakilisha kambi ya weusi na hususani Kaskazini anapotokea. Anazo tracks nyingi ambazo zimewahi kutamba na hadi hii leo akiingia kwa steji na kuanza nazo,basi watu hukubaliana naye.


Hapa anakuja na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina Manuva.Kwanini Manuva,anamaanisha nini?Msikilize hapo chini katika kitu hiki kutoka Mandugu Digital chini ya Dunga.

JOH MAKINIMANUVA


Posted by Bigie on 6:10 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.