BINTI ALIYETAKA KUJIUA KISA KIFO CHA KANUMBA ATOA KAULI NYINGINE......
JAMII 2:17 AM
Binti alietaka kujiua kisa kifo cha Marehemu Steven Kanumba ametaja kitu kimoja ambacho kinaweza kumuepusha kufanya alichotaka kufanya kwa sababu bado ana machungu ya kifo cha mwigizaji huyo.
Mariam ambae aliachiliwa juzi na polisi baada ya kushikiliwa kwa saa kadhaa kutokana na kutaka kujiua amesema “pengine labda nitakapo kaa karibu na waigizaji wenzake kidogo labda nitakua na amani lakini nitakapo endelea kuishi kule misugusugu au vigwaza roho yangu bado itakua haina amani kwa sababu nikivuta picha yake siwezi kumsahau kusema kweli”
Mariam mwenye umri wa miaka 19, Amesema kuwa hana uwezo wa kuigiza lakini akiwezeshwa ataweza, na kwa sababu ya Kanumba ataigiza ambapo wakati yupo hospitali kuna dada mwigizaji wa movie za kibongo alimuahidi kumchukua na kumsaidia kwenye uigizaji lakini mpaka sasa hajamuona wala hajapokea simu yake.






