SUDAN U20 KUWASILI LEO MCHANA JIJINI DAR ES SALAAM

Timu ya Taifa ya Sudan (U20) inawasili leo saa 7.25 mchana (Aprili 19 mwaka huu) kwa ndege ya Ethiopian Airlines namba ET 805 ikiwa na msafara wa watu 30. Sudan inatarajia kufikia kwenye hoteli ya Rungwe iliyoko eneo la Kariakoo, Dar es Salaam. Timu hiyo inatarajia kufanya mazoezi leo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Karume, na kesho itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa. Vilevile kesho saa 4 asubuhi kutakuwa na mkutano wa makocha wa Tanzania U20 na Sudan U20 na Waandishi wa Habari saa 4 kamili asubuhi ofisi za TFF.

Posted by Bigie on 2:40 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.